June 20, 2021


 STAA wa timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezman amefanikiwa kuibeba timu yake baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Hungary katika sare ya kufungana bao 1-1.

Katika mchezo huo Hungary ndiyo walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 45 kupitia kwa nyota wao Attila Fiola na kuwafanya waende mapumziko wakiwa kifua mbele.

N Griezmann ambaye alipachika bao la kuweza usawa dakika ya 66 na kufanya ngoma ikamilike kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Ikumbukwe kwamba katika michuano ya Euro 2016 Griezaman alikuwa mfungaji bora baada ya kufunga mabao 6 na Ufaransa ilipoteza kwenye mchezo wa fainali kwa kufungwa na Ureno ambao walisepa na taji hilo.

1 COMMENTS:

  1. Katika timu ambazo sina imani nazo ya kwanza ni uingerza yani siiamin hata kidogo, timu hovyo sana hii ngoma msimu huu inaenda ujeruman au italy au ubelgiji, inagwa bado ngoma ngumu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic