June 20, 2021


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi kwa ajili ya kupambana katika kutimiza majukumu bila kuwasahau mashabiki.

Jana, Juni 19 kikosi hicho kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
 
Bao la Simba lilifungwa na Luis Miqussone ambaye alipiga pigo huru akiwa nje ya 18 na kuipa pointi tatu Simba.

Matola amesema:"Wachezaji wanastahili pongezi kwa kuwa wanafanya kazi kubwa katika kusaka ushindi hivyo ni jambo jema na kubwa kwetu pamoja na mashabiki.

"Mashabiki nao ni watu muhimu kwa kuwa wamekuwa wakitupa sapoti hivyo ninapenda kuwaomba waendelee kuwa pamoja nasi bila kuchoka," amesema Matola.

Kwenye msimamo wa ligi, Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 70 baada ya kucheza jumla ya 28.

2 COMMENTS:

  1. Lugha kama hii ya Matola ya kutoa shukurani kwa wachezaji sijawahi kulisikia kwa kwa watani

    ReplyDelete
  2. Hata sisi itabidi tubadilike. Zile tabia zetu za chuki chuki ni mambo yalopitwa na wakati. Simba mnatupa somo na huo ndio uungwana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic