August 12, 2021

 JITIHADA za vijana wa Azam FC waliokuwa wananolewa na Kocha Msaidizi,  Vivier Bahati katika kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Kagame, ziligonga mwamba jana Agosti 11.



Ni katika mchezo wa nusu fainali iliyochezwa jana, Uwanja wa Azam Complex,  dakika 90 za awali zilimeguka ngoma ikiwa Azam FC 2-2 Big Bullets. 

Bao la mapema la Bright Muthalk dk ya kwanza liliwapoteza wawakilishi wa Tanzania,  Azam FC waliokubali kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo.


Kipindi cha pili waliamka Azam FC na kutengeneza majaribio kadhaa na iliwabidi wasubiri mpaka dk ya 67 kupachika bao la usawa kupitia kwa Paul Peter. 

Kasi ilizidi kuwa kubwa kwa vijana hao ambapo dk ya 74 nyota wao mwingine Oscar Masai alipachika bao la pili kwa Azam FC.

Bao hilo lilidumu dk mbili pekee kwa kuwa makosa ya safu ya ulinzi yalimpa manufaa Bright tena akapachika bao la usawa dk 76 na kufanya ubao wa Azam Complex kusoma Azam FC 2-2 Big Bullets. 

Zilipoongezewa dk 30 hakukuwa na mbabe na Azam FC ilitolewa katika changamoto ya penalti ambaoo ilifunga 2-4 Big Bullets ambao watacheza fainali Jumamosi na Express ambao waliwatoa KMKM.

Bahati amesema kuwa vijana wake walipambana katika kusaka ushindi ila makosa ya kipindi cha kwanza yaliwagharimu na kuwafanya washindwe kushinda mchezo huo.

8 COMMENTS:

  1. Michezo ya Kimataifa tuwaachie Simba. Ambao wenyewe huwa wanawaita mikia

    ReplyDelete
  2. Kipoteza. kwa Azam kumenisikitisha sana. Tumeshuhudia soca safi kwa pabde zote mbili bila utumizi wa ubabe au malalamiko ya ovyo

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli Azam wametutukana Yanga kistaarabu. Mpira wao safi ni tofauti na sisi tunaotumia pigapiga na faulo zisizo na msingi. Nawaona Azam mbaali shirikisho afrika. Na sisi yanga raundi ya kwanza ama ya pili ndio hivyo tena

    ReplyDelete
  4. We huwezi kuwa YANGA, utaemddlea kujiita yangu ila utabaki kuwa nguruwe fc tu au machupi fc

    ReplyDelete
  5. Ukisema machupi fc unanikumbusha tulivyopigwa na Simba kuke kigoma na Simba ikatwaa ubingwa mbele yetu. Acha kabisa hilo jina aisee

    ReplyDelete
  6. Utopolo na azam mumetuaibixha xana tumemuachieni muchukuwe kombe la mbuzi mukazingua ubora wenyewe tungeingiria kati kingeeleweka

    ReplyDelete
  7. Huna akili si bora yanga na Azam wameshiriki nyie mikia mbona mmekimbia? Vibabu onyango vimekata pumzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic