Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 16
waliochaguliwa katika maboresho ya timu ya taifa, Taifa Stars kwenye hoteli ya
Hill View jijini Mbeya.
Wachezaji hao ni kipa Benedicto
Tinoko Simwanda (Temeke), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na
Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba
(Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili
(Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini
Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na
Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini
Magharibi), Paul
Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana
Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga
Atanas Fabian (Mbeya).
Alisema mpango huu wa kuboresha timu
ya Taifa ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni endelevu na
kusisitiza kuwa hata wale 18 walioachwa watafuatiliwa na TFF na kuitwa
panapokuwa na mahitaji.
“Hawa wote wapo kwenye database ya
TFF na hawataachwa tu hivi hivi wapotee,” alisema kocha Mayanga.
Wachezaji ha0 waliingia kambini mjini
Tukuyu, Machi 21 mwaka huu na wamefanya mazoezi kwa pamoja kwa karibu wiki nne
sasa kabla ya kuchujwa.
Wachezaji 16 waliochaguliwa
wanatarajiwa kuondoka Tukuyu kesho (Aprili 18 mwaka huu) na kwenda kwenye kambi
ya Taifa Stars katika Hoteli ya Kunduchi ambapo wataungana na wachezaji wa
Taifa Stars wa siku zote.
Baadaye watachujwa tena ili ipatikane
timu moja ya Taifa iliyoboreshwa.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia ya Kilimanjro Premium Lager inaunga mkono utaratibu huu wa maboresho ya
Taifa na imewekeza zaidi ya dola milioni 2 kwa mwaka kudhamini Taifa Stars. Huu
ndio udhamini mkubwa zaidi ambao Stars imewahi kupata tangu kuanzishwa kwa TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment