Straika nyota wa
TP Mazembe ya DR Congo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana
Samatta, amesema kinachoifanya Stars isifanye vizuri, suala la wachezaji wengi kung'ang'ania kucheza nyumbani, linachangia.
Hivi karibuni
Stars iliambulia sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Msumbiji, matokeo ambayo siyo
mazuri kwa timu hiyo ambayo Jumapili itacheza mchezo wa marudiano nchini
Msumbiji.
Samatta amesema kuwa ili Stars iweze kufanya vizuri, ni
lazima wachezaji ambao wanakipiga kwenye timu za hapa nchini na kupata
mafanikio, waende kutafuta timu nyingine nje ya nchi ili kuongeza viwango vyao
ambavyo vitakuja kuisaidia Stars.
“Naweza kusema tunashindwa kufanya
vizuri kwa sababu wachezaji wetu wengi wanang`anga`nia kucheza soka la nyumbani
na wala hawajitumi kutafuta nafasi za kucheza soka la kulipwa nje ya nchi,
hivyo ni lazima mastaa wote wakatafute nafasi kwenye soka la kulipwa ili tuweze
kupata maprofesheno wengi wa kuisaidia Stars,” alisema Samatta.
0 COMMENTS:
Post a Comment