April 11, 2020

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amefunguka kuwa bao ambalo walifungwa na Yanga kwenye mechi ya Dabi ya Kariakoo Machi 8, aliliangalia kwenye Makundi ya WhatsApp baada ya kushindwa kutazama mechi hiyo.

Manara amesema kwamba bao hilo alishindwa kulitazama kwa sababu alizima simu zake ambazo zilikuwa na uwezo wa kutazama mechi hiyo. Wakati wa mechi hiyo Manara alikuwa nchini Hispania.

Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison na kuifanya Yanga kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 Manara amesema kwamba mechi nzima kati ya timu hizo aliifuatilia kwa kupitia komenti za makundi ya WhatsApp baada ya kuzima simu ambayo alikuwa akiiangalia mechi hiyo mwanzoni tu mwa mechi kabla ya kufungwa.

"Baada ya mechi kuanza nilizima simu ambayo nilikuwa ninaangalia mechi, nikabaki na simu ambayo watu walikuwa wanachati kwenye magroup, nilipoona kelele zinazidi nikajua tumefungwa na baadaye nikamini tutarudisha haikuwa hivyo," amesema.

10 COMMENTS:

  1. Ila wewe mwandishi sio bure, hii habari si ulishaileta humu kwa tittle nyingine? Shida yako utangaze morrisson tuu!

    ReplyDelete
  2. Hilo ndilo tatizo la waandishi walioishiwa ubunifu ktk blog yake.

    ReplyDelete
  3. Hilo ndilo tatizo la mwandishi aliyeishiwa ubunifu ktk blog yake

    ReplyDelete
  4. Michezo kusimama haimaanishi uwe unatuletea habari ileile

    ReplyDelete
  5. Salehe unatakiwa ujue kuwa blog yako imejaza washabiki wa simba, kwahiyo huku andika habari nzuri tu za simba na mbaya za Yanga. Maana naona kila unpomtaja Morrison watu wanatamani wakumeze.

    ReplyDelete
  6. Nyie mmeishiwa ya kusema ni bora Mnyamaze kimya, porojo linachefuwa Roho, kwanini hamjikumbushi pale Kagera ilipoichapa Gongonje tatu Bila?

    ReplyDelete
  7. Andika unavyojiskia coz wengne hatukuiyon hyo habar Kwan lazma uisome

    ReplyDelete
  8. Kwani hata huko yanga kuna mchezaji mmoja tuu?

    ReplyDelete
  9. Ukiona habari haikuvutii tafuta inayo kuvutia.
    Kala habari lazima itAkua na pande mbili, wanayoipenda na wasio ipenda, kutaka mwandishiaanndike unacho penda wewe Ni Jambo lisiliwezekana...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic