Makocha 35 wameteuliwa kushiriki kozi ya ukocha
ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) itakayofanyika mjini
Morogoro kuanzia Novemba 5 hadi 19 mwaka huu.
Kozi hiyo itaendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday
Kayuni na itafanyikia Mchikichini College ambapo washiriki wote wanatakiwa
kuwasilisha vyeti vyao vya ukocha vya ngazi ya Kati (Intermediate) pamoja na
vyeti vya kitaaluma vya elimu ya sekondari (academic).
Washiriki wa kozi hiyo ni Abdulmaliki Nemes
(Airport FC), Ahmed Haule (Kilimanjaro Talented Youth Sports Centre), Ally
Jangalu (Moro Kids), Amri Saidi (Mwadui FC), Athuman Kambi (Morogoro), Charles
Mwakambaya (Burkina Faso FC), Damian Mussa (Alliance One) na Daudi
Sichinga (Kasulu United).
Denis Maneva (Shule ya Msingi Logo), Edgar
Juvenary (JUT- Mlale), Hamisi Mangolosho (Shule ya Msingi Mtimbwilimbwili),
Henry Ngondo (Chalinze Academy), Issa Hamisi (Polisi Kilimanjaro), Jumanne
Chale (Dar es Salaam), Kizito Mbano (Masasi Alliance), Martin Saanya (Magereza
Morogoro) na Masoud Gumbwa (Sokoine University Academy).
Mbwana Makata (Oljoro JKT), Mrage Kabange (Kagera
Sugar), Muhibu Muhibu (Stand United FC), Nsubuga Solomon (Kishoto FC),
Nyamtimba Muga (Kizuka Secondary), Oscar Mirambo (Makongo), Rashid Abdallah
(Tech Fort Academy), Renatus Shija (Rhino Rangers), Safari Nyerere (Elimu
Sports Academy) na Said Lyakuka (Kizuka Stars).
Simeon Mwesa (Mtibwa Sugar U20), Simon Shija
(Tabora), Suleiman Mtungwe (Ruvu Shooting), Swalehe Allawi Abdul (Alliance
Academy), Yasin Bashiri (Kick Off Sports Academy) na Zuberi Katwila (Mtibwa
Sugar).
Wakati huo huo, kutakuwa na kozi ya wiki mbili ya
ukocha ya ngazi ya Kati (Intermediate) itakayofanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia Desemba 29 mwaka huu.
Makocha wote wanaotaka kushiriki kozi hiyo
wanatakiwa kutuma maombi katika Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania
(Tafca).
0 COMMENTS:
Post a Comment