October 30, 2014


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (Safa) kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na nahodha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini 'Bafana Bafana', Senzo Meyiwa.


Ametuma salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa Safa, Danny Jordan na kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.

Rais Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa mpira wa miguu.

Amewaomba Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.

Rais Sata ,77, alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili mjini Vosloorus.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic