Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu
za rambirambi vyama vya mpira wa miguu vya Zambia (FAZ) na Afrika Kusini (Safa)
kutokana na vifo vya Rais Michael Sata na nahodha wa timu ya taifa ya Afrika
Kusini 'Bafana Bafana', Senzo Meyiwa.
Ametuma
salamu hizo kwa Rais wa FAZ, Kalusha Bwalya na Rais wa Safa, Danny Jordan na
kuongeza kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za vifo vya ghafla vya Rais Sata
na kipa huyo wa Bafana Bafana vilivyotokea wiki hii.
Rais
Malinzi amesema kuwa misiba hiyo si pigo kwa Zambia na Afrika Kusini pekee bali
Afrika kwa ujumla kwa vile walikuwa na mchango mkubwa kwa ustawi wa mchezo wa
mpira wa miguu.
Amewaomba
Rais Jordan na Rais Bwalya kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya
Sata, na familia ya Meyiwa, na kuzitaka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo mizito kwao.
Rais
Sata ,77, alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya King Edward VII nchini
Uingereza alipkuwa kwenye matibabu, wakati kipa Meyiwa aliuawa kwa kupigwa
risasi Jumapili mjini Vosloorus.
0 COMMENTS:
Post a Comment