November 21, 2014

NIYONZIMA KAZINI...
Uongozi wa Simba umekiri kuwa, hauna tatizo katika kumsajili kiungo wa Yanga, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima lakini utafanya hivyo ikiwa tu kocha mkuu wa Simba, Patrick Phiri, atasema anamhitaji.


Niyonzima amebakiza miezi mitano kumaliza mkataba wake na Yanga na ameshatangaza kuwa yupo tayari kuondoka klabuni hapo kama akipata ofa nzuri.
 
AVEVA
Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema wanakubali uwezo wa Niyonzima akiwa uwanjani na wakiambiwa tu anahitajika Msimbazi basi hawatasita kumsajili mchezaji huyo.

“Kilichokuwa kikisubiriwa ni ripoti ya kocha kuona inasemaje, tutawasajili wachezaji ambao atawapendekeza, hata kama akimtaja Niyonzima hatutakuwa na shida, tutamsajili kwani ni mchezaji mzuri.

“Tutaangalia na bei anayohitaji mchezaji husika na tukikubaliana naye basi hakuna shida,” alisema Aveva.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic