Katika kuhakikisha inafanya vema kwenye Ligi
Kuu Bara, Ndanda FC ya Mtwara imeamua kusajili wachezaji kutoka Burundi na
katika timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
Ndanda inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani
katika msimamo wa ligi kuu, tayari imeshaingia mkataba na kiungo wa zamani wa
Mtibwa Sugar, Masoud Ally Mohamed ‘Chille’ ambaye kwa sasa anaichezea Zanzibar
Heroes.
Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mashambuliaji,
Indeshyme Dumu raia wa Burundi ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini
Djibouti.
Katibu wa Ndanda, Selemani Kachele ameliambia
Championi Ijumaa kuwa, nia yao ni kusajili wachezaji sita wakati huu wa dirisha
dogo.
“Lengo letu ni kuhakikisha tunaiboresha timu
yetu kabla ya ligi kuanza kwa kuhakikisha tunasajili wachezaji wenye kiwango,”
alisema Kachele. KATIKA kuhakikisha inafanya vema kwenye Ligi Kuu Bara, Ndanda
FC ya Mtwara imeamua kusajili wachezaji kutoka Burundi na katika timu ya taifa
ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
Ndanda inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani
katika msimamo wa ligi kuu, tayari imeshaingia mkataba na kiungo wa zamani wa
Mtibwa Sugar, Masoud Ally Mohamed ‘Chille’ ambaye kwa sasa anaichezea Zanzibar
Heroes.
Klabu hiyo imeanza mazungumzo na mashambuliaji,
Indeshyme Dumu raia wa Burundi ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini
Djibouti.
Katibu wa Ndanda, Selemani Kachele amesema nia yao ni kusajili wachezaji sita wakati huu wa dirisha
dogo.
“Lengo letu
ni kuhakikisha tunaiboresha timu yetu kabla ya ligi kuanza kwa kuhakikisha
tunasajili wachezaji wenye kiwango,” alisema Kachele.
0 COMMENTS:
Post a Comment