November 28, 2014


Straika wa Simba, Paul ‘Modo’ Kiongera, ametoa mpya baada ya kudai kuwa eti hajui chochote kuhusu yeye kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu ya goti.


Hivi karibuni Simba ilitoa tamko kuwa ipo kwenye mpango wa kumsafirisha Kiongera kwenda India kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kusumbuliwa na goti, kiasi cha kushindwa kuitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara ambayo tayari zimeshachezwa mechi saba.

Kiongera amesema licha ya fununu hizo, yeye binafsi hafahamu kitu chochote kuhusiana na kupelekwa India.

“Mimi sijapewa taarifa yoyote kuhusiana na safari ya kutaka kupelekwa India na uongozi wa Simba kwa ajili ya matibabu ya goti.

“Sifahamu kitu chochote kuhusiana na hilo kwa sababu matibabu yangu nilikuwa nafanyiwa katika Hospitali ya Muhimbili hapa Bongo,” alisema Kiongera wakati alipokuwa katika mazoezi na wenzake kwenye Gym ya Chang’ombe jijini, jana.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic