November 28, 2014


Klabu ya Simba imeshindwa kumsajili chipukizi, James Msuva ambaye ni mdogo wa winga wa Yanga, Simon Msuva.
Tatizo lililochangia kushindwa kumsajili ni kuchelewa baada ya Msuva kuwa amekataa kusaini hapo awali.


Msuva mdogo ameonyesha uwezo mzuri lakini ilielezwa wakati Simba walipotaka kumsajili, akagoma akidai anataka kwenda Ulaya.

Akielezea sababu za kutopewa mkataba kwa mchezaji huyo, meneja wa kikosi cha vijana (Simba B), Patrick Rweyemamu, alisema James hakupewa mkataba mwaka huu, kutokana na taratibu za mikataba yao kumbana kwa kuwa awali alikataa mwenyewe.

“Bahati mbaya ni kuwa alikuwa ameshachelewa kwani tayari usajili ulikuwa umekamilika na hivyo anatakiwa kusubiri mpaka mwakani,” alisema Rweyemamu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic