November 23, 2014


Kiungo mpya raia wa Brazil Emerson De Oliveira Neves Rouqe, anatarajiwa kuwasili nchini Jumatano mchana.



Kiungo huyo ndiye atachukua nafasi ya mshambuliaji Gielson Santana 'Jaja' ambaye ameamua kutorejea nchini.

"Kweli wanatarajiwa kuwasili nchini Jumatano mchana," alisema Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu.

Awali ilielezwa, Emerson angewasili nchini Jumanne akiongozana na Kocha Marcio Maximo pamoja na kiungo Andrey Coutinho.

Hata hivyo, Emerson mwenye miaka 24, atapewa nafasi hiyo ya Jaja iwapo atafuzu majaribio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic