November 23, 2014


Shirikisho la Soka la Namibia (NFA), limeendelea kuonyesha nia ya kumpata Kocha Patrick Phiri kukinoa kikosi chake cha timu ya taifa.


Mmoja wa mtandao wa michezo wa Namibia umeandika kuwa NFA imefanya mazungumzo na Phiri kumshawishi ajiunge na kuchukua nafasi ya kocha wa sasa.
MANETTI.

Kwa sasa, Namibia inanolewa na nyota wake wa zamani, Ricarco Manetti ambaye aliwahi kung’ara na Santos ya Afrika Kusini.

Akizungumza kutoka Lusaka, Zambia, Phiri alikiri kwa mara nyingi kuwa aliwahi kuzungumza na uongozi wa NFA, lakini si hivi karibuni.
“Walinieleza nia yao, ndiyo kile kipindi nikaja Tanzania kuinoa Simba.

“Hivi karibuni ni rafiki yangu tu ndiye aliniambia kwamba Namibia bado wananihitaji. Lakini sijazungumza na kiongozi wa NFA,” alisema.

Phiri yuko mapumzikoni kwao nchini Zambia, anatarajiwa kurejea nchini siku chache zijazo kiuendelea na kazi.


Hata hivyo, Phiri hakuwa tayari kuweka wazi anarejea lini zaidi ya kusema: “Ni baada ya siku chache zijazo, nitakueleza nikiwa tayari kuja.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic