November 27, 2014


MATOLA (KUSHOTO), AKIMUONYESHA SAA KIUNGO KISIGA, KWAMBA AMECHELEWA. KATIKA NI MENEJA WA SIMBA, NICO NYAGAWA.
 Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameonyesha hataki kuchukuliwa ‘poa’ baada  ya kumkomalia kiungo Shabani Kisiga na kumtimua mazoezini.

Matola alimfukuza Kisiga mazoezini wakati wakiwa kwenye gym ya Chang’ombe.
Wachezaji wote walikuwa wamefika siku hiyo na Kisiga akachelewa kwa nusu saa.

Matola akasisitiza suala la nidhamu na hasa kwa Kisiga ambaye ni mkongwe.
Usisahau, tayari Kisiga alikuwa ametoka kwenye kesi.
Lakini hakuwa na ujanja zaidi, zaidi ya kuondoka kwa kuwa msimamo wa Matola ulibaki palepale, kwamba kila mchezaji lazima ajali muda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic