December 20, 2014


Maestro midfield wa zamani wa Simba SC, Haruna Moshi ‘Boban’, amekanusha vikali taarifa zilizoibuka hivi karibuni za kulipwa mshahara na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kutua kwenye timu ya Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.


Hivi karibuni, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti taarifa za msanii huyo kujitolea kumlipa mashahara kiungo mshambuliaji huyo aliyetesa akiwa Simba Sh 400,000 kwa mwezi.

Boban alisema kuwa anashangaa kusikia taarifa hizo na hajui zimetokea wapi na kuwataka watu kujua kwamba hazina ukweli hata kidogo.

“Kiukweli nimeshangazwa na taarifa hizo ambazo naziita za uongo, kikubwa ninachojua ni kwamba timu iliyonisajili ndiyo itahusika kwa asilimia zote juu ya maslahi yangu, ila cha kushangaza naona baadhi ya vyombo vya habari vinaripoti vitu ambavyo havipo.

“Watu wanafanya vitu ili mradi kufurahisha nafsi zao, nimejiuliza sana inawezekana vipi nikalipwa na Diamond ambaye yeye ni msanii na mimi ni mcheza mpira,” alisema Boban.


Wakati huohuo, kikosi hicho cha Friends Rangers, leo kitashuka uwanjani kuvaana na Ndanda FC kwenye Dimba la Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere ‘Makurumla’ ukiwa ni mchezo wa kirafiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic