December 18, 2014


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Kpah Sherman ameikataa jezi namba 25 iliyokuwa ikivaliwa na Emmanuel Okwi.
Sherman raia wa Liberia, alikabidhiwa jezi hiyo namba 25 iliyokuwa ikivaliwa na Mganda huyo wakati akikipiga Yanga.

Taarifa zimeeleza kuwa Sherman amepewa jezi namba 9 ambayo aliitumia Danny Mrwanda tokea ametua Yanga siku chache zilizopita na straika huyo wa zamani wa Simba na Polisi Moro, atapewa jezi nyingine.

Sherman aliitumia jezi hiyo mazoezini na baadaye katika mechi dhidi ya Simba ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-0.

Haikuelezwa wazi sababu ya Sherman kuikataa jezi hiyo lakini taarifa nyingine zimesema anaona haina bahati na ana mapenzi na namba 9 aliyokuwa akiitumia barani Ulaya.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic