December 23, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema pointi tatu dhidi ya mechi ya Kagera Sugar itakuwa ndiyo dira mpya kwao kwenye Ligi Kuu Bara.


Phiri amesema kwa kuwa ligi itasimama baada ya mechi hiyo, vizuri washinde na kwenda wakiwa na uhakika kuwa wamerejea kwenye ligi.

"Kisaikolojia ni vizuri kushinda mchezo huo, kwa umuhimu wa pointi pia ni jambo muhimu sana.
"Wachezaji watakapokwenda mapumziko wakiwa wameshinda, basi watajiamini kwamba wako vizuri na wanatakiwa kufanya vizuri zaidi.

"Mchezaji akienda kupumzika, muda mwingi akiwaza kupoteza inaumiza na inaweza kupunguza nguvu yake. Tukishinda, atarejea akiwa anaamini tunaweza kufanya vizuri zaidi.

"Vizuri tushinde mechi hiyo na tumekuwa tukijiandaa kwa umakini na wachezaji wote na watu wangu wa benchi la ufundi wanaelewa umuhimu," alisema Phiri katika mahojiano jana kutoka Zanzibar.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic