March 29, 2015


Kocha Zdravko Logarusic amekumbana na kipigo chake cha kwanza tokea aliporejea nchini Kenya.


Loga aliyewahi kuinoa Simba, sasa anainoa AFC Leopard ambayo ameiongoza katika mechi nne za ligi ya nchi hiyo akishinda mbili, sare moja na sasa kipigo kimoja.

Mechi yake ya kwanza alikwenda suluhu dhidi ya Chemelil, halafu akazishinda Nairobi City 1-0 na Nakuru All Stars 3-1 kabla ya kukutana na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ulinzi inayomilikiwa na Jeshi la Kenya.


Loga pia amewahi kuinoa Gor Mahia ambao ni wapinzani wakubwa wa AFC Leopars anayoinoa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic