March 4, 2015

TULLY (KULIA) AKIZUNGUMZA NA KOCHA WA ORLANDO PIRATES WAKATI SIMBA ILIPOKUWA KAMBINI NCHINI AFRIKA KUSINI, MWISHONI MWA MWAKA JANA.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema mpira umeingiliwa kwa kuwa wanacholalamika Yanga ni sawa na kichekesho.



Ingawa hajawaweka wazi, Tully ameonyesha kulenga maneno yaliyozungumzwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro aliyesema kuwa Simba ilimchezesha mshambuliaji Ibrahim Ajibu 'Kadra' katika mechi dhidi  ya Prisons.

"Nashangazwa sana na kauli, watu wanazungumza, hawajui lolote. Ili mradi tu wanasema, suala la Ajibu lilipitia taratibu zote viongozi wa Yanga wanajua.

"Sasa unasikia mtu anasema mambo ambayo yanashangaza kabisa kuonyesha hajui lolote kuhusu soka, nasema amevamia huku maana watu wa mpira tunajuana," alisema Tully.

Kabla, Muro alitoa malalamiko kuwa Simba ilimchezesha Ajibu ikijua ana kadi tatu za njano jambo si sahihi.

Lakini Simba ikatoa ufafanuzi kutumia kanuni mpya zinazoruhusu kuchagua mchezaji asicheze katika mechi ipi kutokana na uchaguzi wao.

Naye Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto akalifafanua hilo kwa kusema hakuna kosa lolote kwa kuwa mkutano wa pamoja wa viongozi wa klabu, TFF na Bodi ya Ligi ulipitisha kanuni hizo mpya.


1 COMMENTS:

  1. ni vema jerry muro ukageukia siasa au kaakimya kwanza ujifunze kwani ukimya muda mwengine ni busara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic