May 4, 2015

'ABRAMOVICH' AKIMPONGEZA HANS VAN DER PLUIJM MARA BAADA YA KUWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

Mabingwa wa Tanzania, Yanga wamewasili jijini Dar es Salaam, leo na kupokelewa Kiongozi wa Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali maarufu kama Abramovich.

Akilimali alikuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kuwapokea wachezaji, makocha na viongozi wa Yanga waliowasili wakiyokea nchini Tunisia.
Yanga ilikuwa nchini Tunisia kupambana na Etoile du Sahel ambayo iliitoa Yanga kwa kuifunga bao 1-0 na kusonga kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 jijini Dar.
Abramovich alichofanya ni kumpongeza Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm, benchi la ufundi pamoja na wachezaji kwa kazi nzuri.
“Mmecheza vizuri sana, mmeonyesha soka la uhakika. Mmetolewa lakini kila mmoja kaona juhudi zake,” alisema Akilimali.

Wachezaji na makocha wa Yanga waliwasili na kuingia kwenye gari kwenda makao makuu ya klabu hiyo katika makutano ya Jangwani na Twiga ambako walipokelewa kwa furaha na wanachama.

Yanga imeng’olewa lakini ilionyesha soka safi na la ushindani na kuwapa Waarabu hao wa Tunisia wakati mgumu wakiwa kwao.









1 COMMENTS:

  1. Karibuni nyumbani,yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
    Mmefanya vizuri ila bahati haikuwa yenu,na ndio maana wale mabingwa wa kuzomea hawakujipanga barabarani kuzomea,"AU sijui kwa kuwa wanabembeleza ili muwafunge AZAM"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic