May 5, 2015

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewashauri Yanga kujiandaa zaidi kwa ajili ya michuano ya kimataifa msimu ujao.


Rais Kikwete alikutana na wachezaji wa Yanga Dubai wakitokea Tunisia wakati yeye akiwa njiani kwenda Marekani.

Kikwete alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji hao, wengine wakapiga naye picha.

Pia aliwasifia kwa mchezo mzuri huku akisisitiza wanapaswa kujituma zaidi na kujiandaa vilivyo ili msimu ujao wafanye vizuri zaidi.


Yanga ilifungwa bao 1-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia, hivyo kung’olewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 2-1.

1 COMMENTS:

  1. Kwa ujumla Yanga wako vizuri kuanzia wachezaji,makocha,viongozi na kifedha pia.
    Ushauri wasibadilishe kikosi ila wakiboreshe kwa maandalizi mapema.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic