May 25, 2015


Uongozi wa klabu ya Yanga, leo umemtambulisha kiungo wake mpya, Deus Kaseke.
 Kiungo huyo amekabidhiwa jezi namba 4 ambayo imewahi kutumiwa kwa kipindi kirefu na kiungo wa zamani wa Yanga, Athumani Iddi 'Chuji' ambaye sasa ni nahodha wa Mwadui FC iliyorejea Ligi Kuu Bara. Kwa misimu miwili jezi hiyo ilikuwa inabaniwa na beki Rajab Zahir.
Kaseke ametua Yanga akitokea Mbeya City baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 35, jana.
Kaseke ametambulishwa mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo naye kusema amefurahia kujiunga na Yanga.

“Ninahitaji mafanikio, Yanga ni sehemu sahihi, nafurahi kuwa hapa. Ninaahidi kujituma zaidi ili niweze kufanya vizuri nikiwa na Yanga,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic