August 30, 2015




Na Saleh Ally, Kartepe
Kikosi cha Taifa Stars sasa kitaendelea na mazoezi mara moja tu kwa siku kwa siku zote zilizobaki za kambi yake hapa nchini Uturuki.


Stars imeweka kambi ya siku nane hapa Kartepe, Uturuki kujiandaa na mechi yake dhidi ya Nigeria itakayopigwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema watakuwa wakifanya mazoezi mara moja kwa siku wakiwa wamelenga zaidi masuala ya ufundi.

“Sasa tunaangalia ufundi zaidi huku kidogokidogo tunatunza fitness. Pia hatuwezi kufanya mazoezi makali sana kama ilivyokuwa mwanzo kwa kuwa tunakwenda kwenye mechi,” alisema Mkwasa.


Stars inatarajia kurejea nyumbani Tanzania alfajiri ya kuamkia Jumatano na moja kwa moja itapitiliza kwenda kambini hadi itakapocheza dhidi ya Nigeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic