September 3, 2015

BANDA (ALIYEKAA) AKWIA NA DAKTARI WA STARS, MICHAEL YOMBA, SIKU MOJA BAADA YA KUUMIA MAZOEZINI NCHINI UTURUKI.

Kiungo kinda wa Simba, Abdi Banda anaumias ana kuona atakaa nje kwa siku 21 kutokana na kuwa majeruhi.

Banda aliumia wakati akiwa na kikosi cha Taifa Stars wakati kimeweka kambi nchini Uturuki.
Banda amesema anaumia sana lakini hana cha kufanya na analazimika kuvuta subira.
“Hakuna kitu kibaya kama hiki hasa kama unataka kucheza, unataka kushindana na unataka kuisaidia timu yako ya taifa.

“Nikirudi kwenye klabu yangu, pia nitakosa mechi za mwanzo za ligi. Lakini nalazimika kuvumilia, inaniumiza sana,” akusena Banda.


Banda amejiunga na Simba akitokea Coastal Union na amekuwa kati ya vijana wanaochipukia kwa kasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic