September 3, 2015


Wavuta sigara wa jiji la London wamepewa nafasi ya kuchagua mchezaji bora wa dunia kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.


Jiji la London limefanya ubinifu kwa kushirikiana na wanamazingira na sasa watu watatupia vichungi vyao vya sigara kwenye maboksi maalum.

Maboksi hayo yako sehemu mbalimbali jirani na barabara na hali hiyo imeandaliwa ili kupunguza wingi wa vichungi vya sigara vilivyokuwa vinatupwa barabarani hovyo.


Lakini inaaminika itawasaidia wavuta sigara wakati mwingine kutomaliza sigara yote kama wataviona viboksi hivyo kwa kuvitupia ili kupiga kura ingawa haitahusisha Fifa au kuwasaidia Ronaldo au Messi kushinda kweli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic