Beki wa
pembeni wa Simba, Hassani Kessy, amefunguka na kutaja sababu inayomzuia asiongeze
mkataba ni timu hiyo kutoshiriki michuano ya kimataifa Afrika.
Kufikia
mwezi ujao, Kessy atakuwa amebakiza miezi sita katika mkataba wake na kwa
mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), anaruhusiwa kufanya
mazungumzo na klabu nyingine inayomhitaji ikiwemo Yanga ambayo inatajwa
kumuwania kwa ukaribu.
Yanga
itashiriki katika Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi
Kuu Bara msimu uliopita.
Kessy
amesema mipango aliyojiwekea ni kucheza soka la kimataifa nje ya Tanzania na
ndiyo maana amekuwa akisita kusaini mkataba mpya Simba.
“Sifikirii
kuongeza mkataba wa kubaki kuendelea kuichezea Simba katika kipindi kingine,
licha ya viongozi kuhitaji huduma yangu.
“Ninaamini
kama nikipata timu inayoshiriki michuano ya kimataifa, basi bila kuchelewa
nitasaini mkataba ili iwe rahisi kwaku kutimiza ndoto zangu kwa kuwa
nitaonekana kimataifa,” alisema Kessy.
Sidhani kama mawazo yake ni sahihi, kessy bado ni kijana mdogo ambaye anahitaji kushauriwa kwa karibu.
ReplyDeleteKwa nafasi anayopata Simba alitakiwa aitumie na kuipa Simba ubingwa ili waweze kushiriki hayo mashindano ya kimataifa akiwa katika timu ya kwanza ya Simba "first eleven"
Kwa timu zilizokwisha jiimarisha kama Azam Fc na Yanga Sc Hassan Kessy hana nafasi hata kidogo mbele ya wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa kama Shomari Kapombe na Juma Abdul.
Ajifunze kwa Ramadhan Singano, alikuwa lulu Simba , na alikwisha jihakikishia namba katika kikosi cha kwanza, leo hana namba Azam Fc wala hana nafasi tena ya kuitwa timu ya taifa, inaumiza sana, vilabu viaache kuwadanganya wachezaji wadogo na kuwapoteza kabisa katika ramani ya soka kwa ahadi ya fedha za muda mfupi.
Kessy tulia Simba ucheze mpira, ama nenda kakae benchi TP Mazembe, lakini sio benchi la Azam au Yanga.
Dogo anajidanganya
ReplyDeleteAjifunze Kwa singano
ReplyDelete