February 13, 2016



Sasa amekubali. Kocha wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni, amekiri kuwa anakabiliwa na wakati mgumu sana kuinoa timu hiyo kwani wachezaji wake wengi hawana uzoefu.

JKT Ruvu ambayo katika mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara wikiendi iliyopita ilifungwa mabao 4-0 na Yanga, sasa inashika mkia katika ligi hiyo ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 18.

Kibadeni alisema; “Ni kazi ngumu sana kuinoa JKT kwani nimeikuta imeshasajili wachezaji ambao wengi wao hawana uzoefu, hivyo napata wakati mgumu kuwapa maelekezo.”

Licha ya kumpata Kibadeni kwa ajili ya kuokoa jahazi, lakini JKT Ruvu imekuwa ikisonga kwa mwendo wa kusuasua kabisa.

Kwa sasa katika msimamo wa Ligi Kuu Bara iko katika nafasi ya 16 kati ya 16 kwa ufasaha unasema kusema inashikilia mkia ikiwa na pointi 13, tofauti ya pointi 30 na Yanga iliyo kileleni na pointi 43!


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic