February 7, 2016


Kocha Jackson Mayanja amesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, leo.

Simba inawavaa Kagera Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

“Kagera wana timu nzuri, tunajua watakuwa wagumu zaidi kwa kuwa hawako katika nafasi nzuri, tunalijua hilo.

“Lakini tutajituma zaidi ili kupata matokeo mazuri katika mechi hiyo,” alisema Mayanja raia wa Uganda.

Kikosi cha Mayanja kikosi katika nafasi ya pili kikiwa na pointi 39 wakati Kagera imetylia katika nafasi ya 12 ya msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 15.

Ilipo Kagera ni katika sehemu ya hatari, yaani janga la kuteremka daraja.

Simba iliwasili juzi mjini Shinyanga ikitumia basi lake tayari kabisa kwa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kuona kama Simba inaweza kuendeleza kasi yake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic