February 7, 2016


Kufanya kazi Ulaya ni raha sana kwa maana ya kupiga hatua, lakini nako kuna ugumu wake kimaslahi kama utalifikiria suala la kodi.

Mshambuliaji mpya wa KRC Genk, Mbwana Samatta atakuwa akilipwa mshahara wa euro 35,600 (zaidi ya Sh milioni 85) kwa mwezi.

Lakini makato ya kodi, kupitia kwa Mamlaka ya Kodi ya Ubelgiji, yanamfanya Samatta kuondoka na kiasi kidogo tu cha kodi.

Taarifa za uhakika kutoka Ubelgiji zinasema, Samatta atakuwa akikatwa asilimia 48 kama utajumlisha ‘TRA ya huko’ na makato ya mshahara ya serikali ya mshahara wake. makato ambayo wanakumbana nayo wageni wengi wanaofanya kazi nchini humo.

Pamoja na kulipwa zaidi ya Sh milioni 85, maana yake Samatta atakuwa akipokea euri 18,200 (zaidi ya Sh 38,584).

kabla ya kutua KRC Genk, alikuwa akipokea kitita cha dola 15,000 (zaidi ya Sh milioni 32) kutoka kwa TP Mazembe ambayo aliitumia vizuri kujitangaza.

Maana yake kwa mshahara atakaokuwa akichukua Samatta inaonekana hakuna tofauti kubwa sana na ule aliokuwa akichukua TP Mazembe.

Lakini inawezekana alichoangalia zaidi ni suala la hatua kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi hapo baadaye kimshahara pia kiuchezaji kwa ajili ya kutimiza ndoto zake.

KWa sasa, Samatta ni mwanamichezo anayeshika nafasi ya pili kwa kulipwa mshahara mkubwa nyuma ya Hasheem Thabeet ambaye alikuwa akichukua mshahara hadi dola 200,000 kwa mwezi wakati akikipiga ndani ya NBA na sasa hata kama amepunguziwa kwa kuwa yuko ligi ya chini, haiwezi kuwa chini ya dola 100,000 kwa mwezi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic