August 7, 2016


Kumekuwa na taarifa kuwa Yanga haikutuma majina ya wachezaji wake katika Mtandao wa Usajili wa Kimataifa (TMS) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekaririwa likithibitisha hilo.

Lakini uongozi wa Yanga, umesema taarifa hizo ni zinaonyesha wazi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepanga kuendeleza vita dhidi ya Yanga.

“Tumesikia wanasema hatujatuma majina, nafikiri yamewasilishwa kwao zaidi ya mara moja. Kama unakumbuka sisi tunashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.

KATIBU MKUU WA YANGA, BARAKA
“Kila mmoja anajua kwamba unatuma majina kwenye TMS na TFF pia Caf. Sasa vipi yasiwepo kwao, au wanaficha makusudi ili kutuingiza kwenye matatizo kwa makusudi.

“Inawezekana wanafanya hivyo ili kuivuta Yanga mezaji kwa lengo la kuikomoa. Sisi tuko tayari kupambana hadi haki yetu ipatikane.

“Nakukumbusha, TFF inalijua sakata la Kessy na kwamba wamesema usajili wake haujakamilika. Walijua vipi Kessy sasa yuko Yanga bila ya sisi kupeleka jina lake katika listi ya majina pamoja na hiyo TMS.

“Wamemruhusu Obey Chirwa pia baada ya kumuona kwenye listi ya majina yetu ya Caf pamoja na ligi. Nashangaa TFF nayo imekuwa mshindani wa Yanga utafikiri nayo ni klabu,” alieleza mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye amesisitiza, hawatakubali na TFF wanapaswa kujua Yanga si klabu ya kuonewa.

TFF na Yanga zimekuwa katika mgogoro mkubwa, kila upande ukipambana na mwingine.

TFF ilianza kuonyesha hasira zake baada ya Yanga kuwaruhusu mashabiki wa soka kuingia bure katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.


Lakini kama haitoshi Yanga ikapitisha suala la malipo kufanyika kwa hundi katika mechi dhidi ya Medeama, jambo ambalo lilizidi kuikera TFF, jambo ambalo linaonyesha kuzidi kuamsha hali ya sintofahamu kati ya Yanga na shirikisho hilo ambalo linaongozwa na Rais Jamal Malinzi na Katibu wake, Mwesigwa Celestine, wote waliwahi kuwa makatibu wakuu wa Yanga kwa nyakati tofauti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic