October 19, 2016


FULL TIME: Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga inashinda mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Chirwa na Msuva.
 
Dakika ya 90 + 3: Yusuf wa Toto anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Niyonzima.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza.
 
Dakika ya 88: Chirwa anakosa nafasi ya wazi baada ya kupiga shuti linalotoka pembeni kidogo ya lango.
 
Dakika ya 87: Frank Sekule wa Toto anaingia, anatoka Waziri Jr.
 
Dakika ya 87: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Msuva, anaingia Matheo Antony.
 
Dakika ya 82: Toto wanapata kona, inapigwa na Dida anaudaka mpira lakini kidogo aingie nao ndani, anautoa haraka na kuupiga mbele.
 
Dakika ya 80: Yanga wanafanya mabadiliko, ametoka Ngoma, ameingia Thaban Kamusoko.
 
Dakika ya 78: Toto wanafanya mabadiliko, anatoka Jafar Mohammed anatoka anaingia Soud.
  
Dakika ya 75: Mchezo umechangamka, kasi imeongezeka, Toto wameanza kushambulia kwa kasi lakini Yanga nao wanajibu mapigo.
 
Dakika ya 72: Yanga wanapata kona, anapiga Niyonzima lakini inaokolewa.

Dakika ya 68: Toto wanafanya shambulizi kali, linapigwa shuti kali, Dida analipangua lakini kabla ya wachezaji wa Toto hawajafika, anaufuata mpira na kuudaka tena.
 
Yanga inaongoza mabao 2-0 hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Dakika ya 55: Msuva anapiga GOOOOOOOOO!!!
Dakika ya 54: Wachezaji wa Toto wanalalamika lakini mwamuzi anaweka kati, anaenda kupiga Simon Msuva.
 
Dakika ya 54: Yanga wanapata penalti baada ya Kaseke kuchezewa faulo ndani ya eneo la 18 la Toto.
Dakika ya 46: Waziri Jr wa Toto anafanya shambulizi kwa Yanga, lakini anashindwa kuitumia nafasi vizuri, mpira unatoka nje.
 
Dakika ya 44: Niyonzima anawatoka viungo wa Toto lakini wanamdhibiti na unatoka nje unakuwa wa kurushwa kuelekea lango la Toto.

Kipindi cha pili kimeanza. 

HALF TIME: Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza kipindi cha kwanza.
 
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 43: Toto wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Yanga, anapiga shuti kali lakini linatoka nje ya lango.
 
Dakika ya 41: Beki wa Yanga, Oscar Joshua anaupiga mrefu unamfikia Niyonzima ambaye anachezewa faulo.
 
Dakika ya 38: Toto wanafanya shambulizi kwa 'counter attack' lakini wanashindwa kutumia nafasi hiyo vizuri mabeki wa Yanga wanaokoa.
 
KADI: Dk 33, Ramadhani Malima analambwa kadi baada ya kumuangusha Msuva
Dakika ya 32: Msuva anafanyiwa faulo, Msuva bado yupo chini akipatiwa matibabu na watu wa huduma ya kwanza.
 
Dakika ya 29: Chirwa anaipatia Yanga bao la kwanza, anaunganisha mpira kwa kichwa ni baada ya kupokea pasi kutoka kwa Simon Msuva. Yanga inaongoza bao 1-0.
 
GOOOOOOOOOO!! Chirwaaaaa
 
Dakika ya 26: Niyonzima ambaye ndiye nahodha wa Yanga kwenye mchezo wa leo, anawapa neno wenzake kupambana kwa nguvu huku akizunguka katikati ya uwanja.

Dk 25, Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Junior na Yanga wanaokoa
Dk 22, Niyonzima anawachambua mabeki wawili wa Toto African na kutoa pasi safi kwa Kaseke lakini Carrlos anaokoa
Dakika ya 15: Toto wanafanya shambulizi lakini kabla ya kufikia kipa, Vicent Andrew 'Dante' anaokoa.

Dakika ya 8: Yanga wanamiliki mpira muda mwingi, wanapata faulo lakini wanashindwa kuitumia vizuri.

Dakika ya 3: Timu bado zinasomana, mchezo unachezwa kwa kasi ndogo.
 
Dakika ya 1: Mchezo umeanza hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
 
Timu ndiyo zinaingia uwanjani muda huu.
 
Baada ya kupasha misuli kwa dakika 15, sasa hivi wachezaji wa pande zote wameingia vyumbani ili kumalizia maandalizi kabla ya kutoka nje kuja dimbani kukipiga.
  
Tayari timu zote Toto na Yanga zimeshaingia uwanjani kupasha misuli. Walianza kuingia Yanga kisha Toto nao wakafuatia.
  
Mchezo wa Ligi kuu Bara kati ya Toto Afrcians dhidi ya Yanga unatarajiwa kuanza saa 10:30 jioni ya leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba hapa jijini Mwanza. SALEHJEMBE inakuletea live matukio yote mwanzo mpaka mwisho kuhusu mchezo huo.

KIKOSI CHA YANGA kitakachocheza leo;
1. Deo Munish Dida
2. Hassan Kessy
3. Oscar Joshua
4. Vicent Andrew
5. Kelvin Yondani
6. Mbuyu Twite
7. Simon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Dolnad Ngoma
10.Obrey Chirwa
11. Deus Kaseke

AKIBA:
1. Beno Kakolanya
2. Haji Mwinyi
3. Nadir Ali Haroub
4. Saidi Makapu
5. Thaban Kamusoko
6. Anthony Mateo
7. Juma Mahadhi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic