September 25, 2017



Aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji leo Jumatatu amejitetea  mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuhusu kesi yake ya dawa za kulevya inayomkabili.

Kesi hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa upande wa ushahidi kuanza kutoa utetezi wao ambao leo imekuwa ni siku ya kwanza  kwa mashahidi watatu akiwemo Manji mwenyewe.

 Licha ya mwenyekiti hiyo wa zamani wa Yanga na diwani wa kata ya Mabagala KUU  kutoa utetezi wake wengine walikuwa Daktari wa Hospital ya Aga Khan, Profesa Mustapha Bapumia na bingwa wa magonjwa wa Toto, DR Khan.


Katika utetezi wake,  akiongozwa na Wakili wake, Hajra Mungula, Manji ameieleza mahakama kuwa anafanya kazi ya ushauri wa Kampuni za kifamilia hivyo anaona hakutetendewa  ya kusikilizwa mbele ya mahakama hiyo.

“Sijatendewa haki na sijasikilizwa mbele ya mahakam, dawa ambazo zinatajwa kwenye hati ya mashitaka, Morphiem na Benzodiazepines ni sehemu ya dawa zangu ninazotumia, nimetumia hata siku niliyohojiwa Polisi, nimechafuliwa sana katika jamii kwani hizo dawa nina uthibitisho wake.

 “Napenda kutoa uthibitisho wa nyaraka za maelezo ya Daktari wangu kutoka Marekani kuhusu dawa hizo ambao ulifika kwa njia ya njia ya (e-mail) na sekretari alitoa nakala wakati nikiwa Hospitali ya Muhimbili, historia yangu ya kiafya siyo nzuri matatizo ya moyo yapo katika ukoo wetu maana nilianza kusumbuliwa nikiwa na miaka 26.”

 Manji pia alieleza mahakama hiyo namna jeshi la polisi lilivyoenda kukagua nyumbani kwake lakini waliamua kuondoka na kompyuta yake ambayo amekuwa akihifadhia nyaraka za biashara zake na kuacha sanduku lililokuwa na baadhi ya vifaa anavyotumia katika matibabu yake.

Aliongeza kuwa Polisi hao waliondoka pia  simu, Viza Card, Bima na saa  hadi leo hii alikuwa  hajarudishiwa kwani yote hayo alifanyika baada ya kutoka kuchukuliwa vipimo vya mkojo kwa mkemia mkuu wa Serikali.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic