February 17, 2018



Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema bado mpango wao wa kumaliza Ligi Kuu bara katika nafasi ya tano uko palepale.

Masau alisema timu hiyo itamaliza katika nafasi ya tano wakati ikiwa katika nafasi ya 14, jambo ambalo wadau liliwashangaza.

Lakini ushindi mfululizo, umeifanya timu hiyo ifikishe pointi 20 na kupaa hadi nafasi ya saba.

“Kama nilivyosema mwanzo, mpango wa kumaliza nafasi ya tano uko palepale na tunaendelea kupambana kweli,” alisema.


Masau ameendelea kusisitiza kwamba wana kikosi bora kabisa ambacho kinawapa nafasi ya kufanya vizuri na tayari wameyafanyia kazi makosa yaliyowaangusha mzunguko wa kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic