February 17, 2018




Beki Mau Bofu pamoja na kufungiwa yuko tayari kukutana na Emmanuel Okwi na kumuomba radhi.

Bofu amefungiwa baada ya kubainika kumpiga Okwi kiwiko, jambo ambalo pia lililaaniwa na wadau wengi wa soka.

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema Bofu hakukusudia na tayari amesema yuko tayari kukutana na Okwi kumuomba radhi.

"Tulizungumza naye sana na inaonekana kijana hakuwa amekusudia, ameomba tumkutanishe na Okwi ikiwezekana," alisema.

"Bovu ni mkimya na muungwana sana, niamini mimi. Pia lazima kila binadamu anafanya makosa na yeye ametaka kupata nafasi ya kumuomba radhi kama itawezekana."


Bofu amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi wa Simba katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 4, 2018 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

1 COMMENTS:

  1. Kitendo alichomfanyia Okwi hakikuwa cha kiungwana. Hata adhabu aliyopewa ni ndogo sana kulinganisha na kosa alilofanya la makusudi kabisa huku mpira ukiwa haupo. Hoja ya kutaka kuomba radhi ni mbinu chafu tu ya kutaka msamaha. Haina haja acha maisha yaendelee mbele kwa mbele ipo siku naye yatamkuta aliyomtendea mwenzie.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic