September 17, 2018




Timu ya Polisi Tanzania inayojiandaa na Ligi daraja la kwanza, Jumatano hii 19/09/2018 itashuka katika uwanja wa TPC Moshi kujipima nguvu na Machava FC.


Kwa mujibu wa Afisa habari na Mawasiliano wa Timu ya Polisi Tanzania Frank Geofray amesema mchezo huo ni moja ya maandalizi ya Ligi daraja la kwanza ambapo Polisi itatumia mchezo huo kuangalia kikosi chake kabdla ya kuanza kwa ligi hiyo ambapo Polisi itaanza kucheza na Mashujaa mkoani Kigoma.


Frank amesema hali ya kambi yao inayoendelea Chuo cha Polisi Moshi CCP ni shwari na Wachezaji na benchi la ufundi wana ari na morali ya kuhakikisha kuwa msimu huu tunafanikiwa kupanda kucheza Ligi kuu Tanzania bara.


"Tunawaomba Wapenda soka wa Mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kuipa sapoti timu hii kwa kuwa hii ndio timu pekee yenye nafasi ya kuifanya Kilimanjaro irejee kwenye anga zake za mpira."


Geofray amesema mwaka huu hawataki makosa ya msimu uliopita  yajitokeze kwa kuwa hawana sababu ya kutokufanya vizuri ukizingatia uwezo wanao

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic