Simba imefanikiwa kupata uhamisho wa Kimataifa
(ITC) wa wachezaji Amis Tambwe na Kaze Gilbert ‘Demunga’.
Mwenyekiti wake, Ismail
Aden Rage alilazimika kusafiri jana kwenda Bujumbura, Burundi kusaka ITC hiyo
na leo mchana alifanikisha suala hilo.
Katika mechi ya jana ya ufunguzi wa Ligi Kuu
Bara, Demunga na Tambwe walishindwa kucheza kutokana na kutokuwa na ITC.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema wachezaji hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya
taifa ya Burundi (Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi Kuu ya
Tanzania Bara na iliwasababishia usumbufu mkubwa.
Rage aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku kwenda kulishghulikisia suala hilo.
"Kila walipokuwa wakipigiwa simu kwa takribani siku tatu mfululizo walikuwa wakisema kwamba wako milimani. Sasa hawa watu wa Burundi wakikwambia wako miliman wanamaanisha wameenda kijijini kwao. Kuongea kwa simu pekee kusingetosha na ndiyo Kamati ya Utendaji ya Simba iliomba niende mwenyewe Burundi ili suala hili liishe," alisema Rage.
Kutokana na ITC hiyo, maana yake timu Warundi hao wataanza kuitumikia Simba katika mechi dhidi ya JKT Oljoro, keshokutwa mjini Arusha.
Taarifa za uhakika zinaeleza chanzo cha
Vital’O kuiwekea Simba ntimanyongo ni kutaka wachezaji hao wacheze michuano ya
Chan nchini Afrika Kusini ambayo Burundi imefuzu baada ya kuing’oa Sudan.
0 COMMENTS:
Post a Comment