Naomba,
kama Ezekiel Kamwaga, kutoa maoni yangu kuhusu sakata la Katibu Mkuu wa Yanga.
Maoni haya hayana chembe ya ushabiki ila ni maoni ya Mtanzania anayependa soka.
Mimi sikubaliani na Ukatibu wa Yanga kupewa Mkenya.
Na nisingekubaliana pia na
Mkenya au Mganda (au raia mwingine yeyote wa kigeni) kuwa Katibu Mkuu wa Simba.
Na hili pia halina uhusiano na ajira yangu ya Simba kwamba ninasema hivi ili kulinda
kibarua changu na Katibu wangu. Siko huko.
Niko kwenye mantiki zaidi.
Nitaeleza. Ninaamini kwamba klabu hizi mbili ni miongoni mwa tunu za taifa letu
la Tanzania.... Watu wanapenda vilabu hivi kuliko wanavyopenda kitu kingine
chochote... Simba na Yanga ni zaidi ya CCM na CUF au CHADEMA..
.Unapomweka pale
mgeni ni lazima kwanza upime na ujue anatoka wapi, anataka nini, katumwa na
nani? Mtu anaweza kuamua kuvuruga amani ya nchi yetu kwa kutumia timu hizi
mbili tu ! Hili ninalolisema nalifahamu vizuri... Pili, ni kweli kwamba hakuna
MTANZANIA mwenye uwezo wa kuongoza Simba au Yanga vizuri?
Nafasi hizi za kazi
huwa zinatangazwa na watu wenye sifa kupeleka sifa zao? Au viongozi wanachagua
vibaraka wao kuongoza badala ya kutafuta watu wenye uwezo ambao naamini wapo
wengi tu? Hivi taifa hili ambalo limemtoa Julius Nyerere, Salim Ahmed Salim,
Joseph Warioba, Nehemia Mchechu, Reginald Mengi, Patrick Ngowi na wengine wengi
halina uwezo wa kutoa Katibu Mkuu tu wa Yanga au Simba? Tujiulize, ni wasomi na
watu wangapi wenye akili zao ambao wanaweza kuja kukubali kufanya kazi Simba na
Yanga kwa sasa? Mazingira yaliyopo sasa yanamfaa mtu mwenye heshima yake kutaka
kufanya kazi Simba au Yanga? Je, Katibu Mkuu ana uwezo wa kubadili mambo na
yakaenda kisasa kwenye vilabu vyetu. Si ni Mwalusako huyuhuyu ambaye alitangaza
Ofisa Habari Mpya na akalazimishwa akanushe taarifa hiyo na baadaye ikatangazwa
Ofisa Habari ni huyohuyo lakini akiwa na baraka za aliyemlazimisha Mwalusako
abadili taarifa? Je, viongozi waliopo sasa haswa hawa watendaji, hawa wa
kuajiriwa kama makatibu na wasemaji, kwenye vilabu hivi, wana nguvu ya kutosha
kimamlaka kuleta mabadiliko yanayotakiwa? Tatizo ni la uraia au mfumo uliopo?
Pia, Kenya wametuzidi nini kwenye soka yao? Huyo anayeletwa ana profile gani
kwenye football? Alifanya nini huko alikokuwa ? Ana sifa gani ya ziada ambayo
hakuna MTANZANIA mwenye nayo? Nasikitika sana kwamba wapo Watanzania
ninaowaheshimu sana ambao wanaona kwamba wageni waje tu kuchukua ajira za
wenyeji. Huu ni UTANZANIA gani? Huu ni UTAIFA gani tulionao.
Huwezi
kulinganisha Simba au Yanga na timu kama Arsenal na Man United ambazo tayari
zinamilikiwa na wageni. HIZI MBILI NI TIMU ZETU NA ZINATAKIWA KUBAKI ZETU..WATANZANIA WA KUFANYA HIZO KAZI WAPO. Kinachotakiwa ni kuboresha mazingira ya
kazi. Kubadilisha mifumo ya vilabu vyetu hivi. Kwa mfumo wetu huu wa sasa, Hata
umlete David Gill wa UEFA atachemsha tu. Ni maoni yangu tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment