October 10, 2021


 UKIACHA bao matata ambao lilifungwa na mzawa Cleophance Mkandala kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Jamhuri Dodoma kuna bao bora limepatikana kwa wakati huu kutoka kwenye miguu ya mzawa Crispine Ngushi wa Mbeya Kwanza.

Hiyo ni kwenye Ligi Kuu Bara kwa mzunguko wa pili ikumbukwe kwamba ligi kwa sasa imesimama na kupisha timu za taifa kucheza mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Timu ya Tanzania, Taifa Stars leo ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Benin huku ikiwa na kibarua cha kusaka ushindi kwa kuwa mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0, Uwanja wa Mkapa.

Kwa waliotupia wengine mabao makali ni pamoja na lile bao la Rashid Juma ambaye aliwatungua Biashara United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara kubwa na lingine ambalo linatajwa kuwa bora lilifungwa na Vitalis Mayanga mbele ya KMC, Uwanja wa Karatu dakika ya 3 kwa shuti lilomshinda mlinda mlango Juma Kaseja.


 Kubwa kuliko yote ilikuwa ni lile lilolufungwa na Ngushi kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.Ngushi alifunga bao hilo kwa mtindo wa Acrobatic akiwa ndani ya 18 na ilikuwa dakika za lala salama mbele ya Mbeya City kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine.


Mzawa huyo pia aliweza kumfunika mshikaji wake William Edgar ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza ndani ya ligi ambapo aliwatungua Mtibwa Sugar kwa shuti kali, Uwanja wa Mabatini,Kibaha.


Nyota huyo wa Mbeya Kwanza aliweza kuyafunika mabao yote 22 ambayo yamefungwa kwa msimu wa 2021/22 kwa kuwa bora na kali ndani ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic