Uongozi wa Yanga umelazimika kukatisha safari ya Kocha Mkuu mpya wa
Yanga, Hans van Der Pluijm kwenda Zanzibar na kumsafirisha kwenda Kigali.
Kocha huyo amepelekwa Kigali haraka leo mchana ili akapande ndege
kwenda Uturuki.
Awali uongozi wa Yanga ulitaka kocha huyo aende Zanzibar na kushuhudia
fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya KCC na Simba.
Lakini kutokana na kukosa ndege ya kuondoka leo, van Pluijm
akasafirishwa hadi Kigali.
Baada ya kutua Kigali na Rwandair, Mholanzi huyo atakwea pipa la
Turkish Airways ambalo litampeleka hadi Istambul.
Atapumzika Istambuli kwa zaidi ya saa tatu kabla ya kuunganisha ndege
hadi Antalya ambako Yanga imeweka kambi.
Kocha huyo mpya amelazimika kuondoka haraka kwenda Uturuki na kuungana
na Yanga kwa kuwa Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa atarejea nyumbani
jijini Dar.
Mkwasa anarejea kwa ajili ya kuja kusherekea zaidi ya miaka 20 ya ndoa
yake na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment