Mwamuzi Andre Marriner amechemsha na kuingia kwenye kundi la waliochemsha
kwenye Ligi Kuu England baada ya kumlamba kadi beki wa Arsenal Kieran Gibbs.
Mwamuzi huyo alimtoa
Gibbs kwa madai ya kushika mpra uliopigwa na Eden Hazard lakini hali halisi
ilikuwa hivi, aliyeshika alikuwa ni Alex Oxlade-Chamberlain.
Pamoja na Chamberlain
kumwambia mwamuzi kwamba aliyeshika ni yeye, lakini hakukuwa na mabadiliko.
Gibbs alitoka
uwanjani akiwa analaumu kutokana na kilichotokea katika mechi hiyo dhidi ya
Chelsea kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London, leo.
Katika mechi hiyo,
Arsenal walizidi kurudi ‘rivasi’ baada ya kupoteza kwa mabao 6-0 na kuzidi
kujiweka nafasi mbaya ya kuwa washindani wa kuwania kutwaa ubingwa.
majanga mbona ingekuwa bongo
ReplyDelete