Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga leo
wameonyesha bado wana nguvu ya kuwania kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya
kuwachapa Prisons ya Mbeya kwa mabao 5-0.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, Yanga walionyesha hawana mchezo baada ya mabao kalamu
hiyo ya mabao kuonyesha wamejirekebisha kutokana na kale kamtindo ka kupoteza
nafasi.
Yanga ilipata bao lake la kwanza kupitia
mshambuliaji nyota Emmanuel Okwi aliyefunga kwa mkwaju wa adhabu. Baadaye Okwi
aliumia na nafasi yake ikachukuliwa na Hamisi Kiiza.
Kiiza alifunga mabao mawili, mengine
mawili yakafungwa na mshambuliaji mwenye kasi, Mrisho Ngassa na nahodha Nadir
Ali Haroub ‘Cannavaro’ ambaye siku hiyo amecharuka katika upachikaji mabao.
Maana yake Yanga imefikisha pointi 46 na
inaendelea kubaki katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment