HAPPY-MILEN MAGASE |
Mwanamitindo na Miss Tanzania 2001, Happiness
Magese amefungua mfuko kwa wanawake kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa tumbo la maumivu uzazi inayojilikana kama ‘Endometriosis’.
Akizungumza kwenye Hotel ya Kempisky, Posta
jijini Dar es Salaam Magese alisema kuwa kwa kupitia mfuko wake wa ‘Millen
Magese Foundation’ atasaidia kuelimisha wanawake ili kujua dalili na matibabu
ya ugonjwa huo.
Magese alisema kuwa, anajua amechelewa kutoa
somo la ugonjwa huo, lakini kwa kupitia makampuni mbalimbali yaliyojitokeza
kumsapoti, anaamini atafanikiwa.
MMOJA WA MADAKTARI AKIZUNGUMZIA UGONJWA HUO |
“Nimefikia hatua hii ya kutoa somo na semina
mbalimbali za ugonjwa huu ni kutokana na kuwahi kuugua na kunitesa muda mrefu
tangu nikiwa shuleni.
“Ninaamini wapo wanawake wengi wanaougua
ugonjwa huu, lakini wanakuwa hawajitambui, lakini kwa kupitia mfuko wangu
niliouanzisha watajitambua.
MENEJA WA MILEN HAPPINESS-MILEN, LUCY NGONGOSEKE. |
“Kwa kupitia mfuko huu, nitaweza kujenga
hospitali maalumu ya wanawake itakayotibu ugonjwa huo ambao bado Tanzania
hawajautambua,”alisema Magese.
Aidha, daktari wa Muhimbili, Belinda
Balandya alisema kuwa ugonjwa huo unawapata wanawake wenye umri kuanzia miaka
25-35 waliopo tayari kubeba ujazito.
Balandya alkizitaja baadhi ya dalili za
ugonjwa huo ni siku chache kabla ya siku za mwanamke (hedhi) damu nyingi
inatoka na mgongo kuuma, maumivu wakati wa tendo la ndoa, maumivu ya mapafu na
kuharisha.Magese alisema kuwa, Jumapili ijayo kwa
kushirikiana na madaktari wa muhimbili ameandaa semina kwa wanawake wanafunzi itakayofanyika
kwenye fukwe za Coco.
0 COMMENTS:
Post a Comment