November 18, 2016


MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI YA SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE AKIWA NA MOHAMED ZIMBWE MAARUFU KAMA TSHABALALA PAMOJA NA BABA YAKE NA MENEJA WAKE, HERY MZOZO.

Uongozi wa Klabu ya Simba, umefikia makubaliano na beki wake, Mohamed Zimbwe Jr ambaye ni maarufu kama Tshabalala.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba Zimbwe ana mpango wa kujiunga na Yanga kwa kuwa mkataba wake na Simba umeisha.

SALEHJEMBE jana lilimshuhudia beki huyo akitua kwenye ofisi za Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe akiwa ameongozana na meneja wake, Herry Mzozo.

Mazungumzo yao yalichukua kama dakika 25, baadaye Zimbwe Jr alitoka nje na baba yake alitoka nje kabla ya kurejea tena ndani na kumalizana.

Baada ya mazungumzo hayo, Hans Poppe alisema walikuwa wamemalizana kwa maana ya makubaliano na kila kitu.
“Sasa tumemalizana na Tshabalala, awali tulizungumza na leo ilikuwa ni kumalizia tu,” alisema Hans Poppe.

Mzozo naye alithibitisha kuhusiana na hilo: “Kweli tumemalizana kwa maana ya nini kifanyike, suala la maslahi na kila kitu. Hapa kilichobaki ni suala moja tu, kusainishana mikataba.”

Baada ya suala la beki huyo wa kushoto, sasa ni suala la kiungo Jonas Mkude ambaye pia amekuwa akielezwa kwamba ana mpango wa kujiunga na Yanga, hata hivyo, Kamati ya Utendaji ya Simba inakutana leo Ijumaa kwa ajili ya kujadili masuala kadhaa lakini la usajili linaonekana kuwa namba moja.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV