May 28, 2014


Mwanamitindo maarufu duniani na Miss Tanzania 2001, Happiness Magese ameonyesha kitendo cha uungwana wa hali ya juu wakati akifungua mfuko kwa wanawake kwa ajili ya kuwatibu ugonjwa wa tumbo la maumivu uzazi inayojilikana kama ‘Endometriosistibu'.


Wakati wa uzinduzi huo, Milen alimkumbuka mwandishi na mpigapicha mahiri, Athumani Hamisi Msengi ambaye sasa hawezi tena kutembea.

Msengi alipata ajali ya gari takribani miaka mitano iliyopita na kusababisha kwisha kwa ndoto zake za kuendelea kufanya vizuri kwenye taaluma yake.

Wakati akiwa anajiweza, Msengi alikuwa kati ya watu waliomsaidia sana Milen hadi kutwaa taji la Miss Tanzania 2001.

Milen ni muungwana, ameweza kumkumbuka mpigapicha huyo kwamba alikuwa na mchango kwake, lakini angalia wangapi leo wamemsahau wakiwemo waandishi wenzake?

Kampuni alizozitumikia na hata ile ambayo alikuwa akiitumikia siku anaingia matatizoni.

Lakini Milen ambaye sasa ni mwanamitindo maarufu ameweza kukumbuka alichokipata kutoka kwa Msengi, akamjumuisha katika semina hiyo aliyoifanya.

Wangapi wana uwezo wa kuwa na moyo kama huo wa Milen, binti huyo 'raia' wa Mwanza, Mtanzania anayeng'ara lakini ameweza kukumbuka mengi.

Tujifunze kupitia kwake, ameonyesha ubora na tukubali kasoro zetu.
Namuomba Mwenyezi Mungu amuongezee Milen zaidi na zaidi kwa kuwa ni mtu anayeweza kukumbuka alikotoka na aliosumbuka nao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic