Pamoja na kutopanda kwenye Ligi Kuu Bara msimu ujao
kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa yupo mbioni
kutimkia nchini Ghana na Nigeria kusaka wachezaji atakaowasajili katika timu yake
msimu ujao .
Mwadui bado inasubiri maamuzi ya Shirikisho la Soka
la Tanzania (TFF) kutokana na rufaa iliyokata kupinga kutopanda daraja kutoka
Daraja la Kwanza kwenda Ligi Kuu Bara, ambapo Stand United ilipewa pointi za
mezani na kuwapiku.
Julio alisema anachojua wao ni mabingwa, hivyo
atafanya usajili wa wachezaji 25, ambapo ni makipa watatu na wachezaji 22 wa
ndani.
“Natarajia kwenda nchini Nigeria na Ghana kutafuta
wachezaji wazuri kwa ajili ya kuwasajili katika kikosi changu ili kujiandaa na
msimu ujao.
“Lengo langu ni kusajili wachezaji wanne wa nje,
washambuliaji wawili, beki mmoja na kiungo mmoja, kwani naamini nchi hizo ndizo
zina wachezaji wazuri, mfano mzuri ni kama Azam ambao wamemsajili Kipre Tchetche
na Balou ambao wamefanya vizuri kwenye ligi,” alisema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment