July 26, 2014



Bondia wa ngumi za kulipwa nchini ambaye ni bingwa wa zamani wa Afrika Mashariki na Kati, Mada Maugo ‘Maugo Jr’, amesema lazima atamuulia ulingoni mpinzani wake Thomas Mashali.


Maugo amesema, asipokufa Mashali, basi naye atafia ulingoni wakati wa tamasha hilo la Usiku wa Matumaini lililopangwa kufanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
MASHALI

 “Hivi ninavyozungumza nipo gym na kocha wangu ambaye amewasili kutoka Nairobi ili kuendelea na maandalizi, cha muhimu ni kumuomba Mungu niwe na afya njema mpaka siku ya ‘game’,” alisema Maugo kwa sauti ya kujiamini.
Maugo na Mashali ni mabondia wenye upinzani wa jadi ndani na nje ya ulingo ambapo watapanda ulingoni kurushiana makonde katika kilele cha Usiku wa Tamasha la Matumaini linalotarajiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic