July 26, 2014



Vita ya maneno! Kauli inayofaa kutumika kwa makocha wa Simba na Yanga ambao wamejibizana kuhusu kambi ya Visiwani Zanzibar.
Siku chache baada ya Kocha wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic, kutaja sababu za kuweka kambi Visiwani Zanzibar, naye Kocha wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo, ametaja sababu kuu tatu ambazo zimemfanya kuomba kuweka kambi visiwani humo kabla ya kuanza kwa ligi kuu.

Maximo, amesema kuwa kikosi chake kitakuwa na kambi Kisiwani Pemba kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali inayowakabili ikiwemo ligi kuu itakayoanza kutimua vumbi Septemba 20.

Maximo alizitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na hali ya hewa ya utulivu, uzuri wa viwanja vyao na muda mfupi uliobakia kujipanga.

Alikwenda mbali na kufafanua kuwa kwa muda huu, ingekuwa vigumu kuweka kambi mbali na Tanzania, hivyo ameamua kuomba kambi karibu ili kufidia muda wa majaribio.

“Zanzibar kuna hali nzuri ya utulivu, viwanja vizuri kwa mazoezi lakini pia unaweza kuangali muda pia tulionao wa kujiandaa, nafdikiri ni suala la ‘kuofa’ muda wa mazoezi, badala ya kwenda mbali na nyumbani,”alisema kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa.
Hata hivyo alishindwa kutaja tarehe maalumu ya kwenda Pemba, ambapo alisema itakuwa baada ya wachezaji wote walio katika timu zao za taifa kurejea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic