MCREGGAN AKIKABIDHIWA MOJA YA KADI ZAKE ZA BIMA.....SHEMEJIIIII |
Kundi maarufu la vichekesho
nchini la The Original Comedy limepata mafanikio mengine baada ya benki ya CRDB
kuwapa bima za aina mbili.
The Original Comedy chini
ya kiongozi wao Sekioni David maarufu kama Seki wamepata bima ya maisha pia
bima ya matibabu au unaweza kusema bima ya afya.
Kupitia kampuni yake mtoto
ya CRDB Microfinance, benki ya CRDB imetoa bima ya matibabu kwa The Original
Comedy kupitia kampuni ya AAR.
BOSI WA COMEDY ORIGINAL, SEKI AKIELEZEA JAMBO |
Lakini pia CRDB imetoa bima
ya maisha kwa The Original Comedy kupitia kampuni ya African Life.
Shughuli nzima ya
kukabidhiana kadi za bima hizo, ilifanyika leo kwenye Benki ya CRDB tawi la
Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Wakati wa makabidhiano hayo,
wasanii wa kundi hilo, Joti, Vengu, McRegan, Mpoki na kiongozi wao Seki
walikuwa katika eneo hilo.
JOTI NAYE AKIPOKEA KADI YAKE YA BIMA... |
Pamoja na wasanii hao kuwa
kivutio, mmoja wa warembo waliowahi kung’ara katika Miss Tanzania, Nargis
Mohammed ambaye ilielezwa ‘anapiga job’ kwenye kampuni ya CRDB Microfinance,
naye alikuwa katika eneo hilo.
“Mbali na kupata matibabu kwenye hosptali bora za hapa nchini
lakini pia wana nafasi ya kutibiwa nje ya nchi kama vile Kenya, Afrika Kusini
na India, hii siyo kwao pekee bali hata kwa familia zao.
“Tumeamua kufanya hivyo
kutokana na kundi hili kuwa bora zaidi hapa nchini hivyo wadau wengi wakishaona
hivyo ikiwa ni pamoja na makundi mengine basi watavutiwa na hali hiyo nao
watataka kupata huduma hii,” alisema Arthur Mosha, Meneja wa kitengo cha Bima,
CRDB.
Naye kiongozi wa kundi la
The Original Comedy, Seki alisema kuwa wameipokea kwa mikono miwili huduma hiyo
waliyopewa ambayo sasa imewapa amani katika maisha yao ya kila siku hivyo
watafanya kazi yao bila ya kuwa na wasiwasi tena.
“Huduma hii pia
imemuhusisha ndugu yetu Joseph Shamba ‘Vengu’ ambaye ni mgunjwa, ila yeye
atapata bima ya maisha pekee na siyo ile ya matibabu.
“Anaweza kupata bima ya
matibabu endapo hali yake ya kiafya itarejea kawaida kama zamani lakini kwa
sasa imekuwa vigumu kutokana na sababu mbalimbali,” alisema Seki.
0 COMMENTS:
Post a Comment